letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de diaspora - roma

Loading...

ooii yooh
tongwe records beiby
(bin laden)

verse 1
umwambie sikupenda, kuikimbia nchi yangu
kabla kalenda nimeondoka kabla ya mwanangu
na sijui ninapokwenda simjui na mrithi w-ngu
usije ukambemenda mwanangu oii

kitovu chake ukizike nilipopitisha unyayo
akiwa wa kike ndo furaha niitakayo
ukinizalia dume inshallah ni hayo
nitampa jina la mtume na nitamuita matayo

akikuwa mwambie babake alikuwa mwanaharakati
na ukamwonyesha ununio ndio k-mbuk-mbu iliyobaki
awaheshimu nduguze ambao walimwachia ziwa
wamthamini wamtunze abadani asijione mkiwa

na asinichukie mimi maana sik-mchukia babu yake
akikuwa atajua kwanini na ataheshimu maamuzi yake
auchunge ulimi aishike dini yamkini ana jini mkongwe
na umsikizishe yangu mapini (ili mjini asikae kinyonge)

na ukipata usimsahau mama, mk-mbuke na bibi
niombee nitusue mnyama, nabeba kago msumbiji
sijui nitapona nitakufa sijui nitarudi
akikuwa mwambie roma ndo baba we ndo shahidi
chorus
uvumilie, utuliе, umlilie
haya maisha ni safari
usilie, uvumilie, utuliе na umlilie
haya maisha ni safari

verse 2
nafahamu utazaa kwa uchungu
leba utalia na mengi akidondoka chini ya uvungu
watambeba malaika wengi
mimba huja na kisirani, na kuna unavyotamani
huku nilivokuta sivo nilivodhani ila siwezi rudia njiani

na unafahamu hunnie ile nyumba ya urithi haina vigae
so unaweza pima mzani ni rudi ama nikomae
bora nikomae tu tujichange tumjengee mama kibanda
inshallah mpaka uzae nitakuwa nimeshajipanga

na nimetuma picha yangu waonyeshe wanangu wasinisahau
waambie baba atarudi uwape moyo angalau
kuna muda nina hamu ya ngono ila sina hisia ya mapenzi
so please ongeza visomo kwa yule ustadh wa mbezi

najua unanimiss ila jitunze nami nitakutunzia fimbo
walinde wanangu wao ndo warithi na ndizo za roma simbo
wananiambia mashabiki roma rudi uchukue jimbo
huku ukizingua polisi tu unaekewa goti la shingo
basi ni hayo tu maisha ni mapambano ila sio sinza
na usisahau kuwapa tano dajide, mada na siza
na uwaambie huku watu hawachagui kazi
ila majungu na umbea yaani vitu ni vingi mzazi

chorus
uvumilie, utulie, umlilie
haya maisha ni safari
usilie, uvumilie, utulie na umlilie
haya maisha ni safari

uvumilie, utulie, umlilie
haya maisha ni safari

tongwe records beiby
(bin laden)

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...