letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de wageni - paul clement

Loading...

difficult but not impossible

katika maisha yangu nilipokea wageni
nikawakaribisha kw-ngu wakafanya vitu vingi
hawakua wa kudumu walikua wapitaji
ila moyo wa ukarimu ukanisababishia machozi

mgeni wa kwanza alikuwa ni uchungu
akaniumiza akanipa maumivu alipomaliza
akaenda zake
mgeni wa pili alikua ni huzuni huyu nae
akanikosesha furaha
mgeni wa tatu alikua ni magonjwa
akanidhoofisha akataka kuniua
hakufanikiwa akaenda zake

aliefuata alininyima watoto, jina lake tasa
nae alipita
mgeni mmoja jina lake ni mauti akamchukua
mtimi akaniachia jeraha
mgeni mwingine jina lake hofu
hakutaka nifanikiwe akanipa fikra potofu
nikajiona siwezi, tena nitafeli
huyo naye alipita

hawa ni wageni, tena wapitaji
hawatadumu, watapita (aah)
hawa ni wageni, tena wapitaji
hawatadumu, watapita

hakuna jambo lolote gumu litakalodumu
kwenye maisha yako
ila yote yatapita na yakishapita
(hayatarudi tena)
tough times never last, but tough people do

mapito sio mambo magumu unayoyapitia
kwenye maisha yako, ila mapito ni mambo
magumu yanayopita katika maisha yako
ndio maana tunayaita mapito kwa maana
yanapita tuu, na yanapita kwenye maisha yako
na yakisha pita, hayawezi kurudi tena aah

magonjwa
hawa ni wageni (tena) tena wapitaji,
(aah) hawatadumu (wanapita) watapita
eeh ii uchungu
hawa ni wageni tena wapitaji (eeh ii), hawatadumu watapita
eh eeh huzuni
hawa ni wageni tena wapitaji, hawatadumu watapita
eeh mateso, changamoto
hawa ni wageni tena wapitaji, hawatadumu watapita
eeh eeh
hawa ni wageni tena wapitaji, hawatadumu watapita aah aah

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...