letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de laana (diss) - fivara

Loading...

ah!
nianze na goats msingeni’inspire ningewa’inspire nyie
hii kauli ka’ ile, “usingenizaa ningekuzaa mie”

naomba mtulie ili dawa iwaingie
na naahidi atakaejibu hii lazima nimrudie

amna mchango zaidi ya kuwa ma’rapper mliopita
mliotangulia na sasa inasikitisha

mambo mnayofanya yanawashusha kabisa
sawa na mama ambae akivaa tu vijana wanadisa

kwanza nyie ni wanafki, wabinafsi
watu wazima mmezidiwa moves hadi na mondi wasafi

hivi hamumuoni jigga? hamumuoni nas?
ebu tuachieni gepu sio kushindana nasi

mnafanya ngoma kiboya ili mbaki kwa chart
style za miaka hii hamuwezi bora tu mka’relax
(relax)

tatizo wengi wenu mshabugi
mbele hamuendi naona nyuma mnarudi
baada ya kuwa moguls nyie mnakuwa chawa
wengine mmeingia hadi bungeni lakini bado mnapagawa

ngoja niseme hii maana naona haiko sawa
legacy yako unafuta mwenyewe kwa kupona madawa

umefanya vitu vikubwa unakosa hata mbawa
unabaki kulalamika unaona hakuna usawa

siwavunjii heshima, heshima mnavunja wenyewe
mnatoa maboko hadi tunauliza, “hii katunga mwenyewe?”

mnafeli pakubwa, nawachana wakubwa
hasheem aligundua mapema basi akastaafu muda

tatizo hamkuwa smart mngekusanya fuba
sasa mnageuka ma’wack hadi tunawaona wakuja

ah!
hata wajinga wanazeeka (ndio)
sio kila mzee ana hekima
mlichofanya kweli mlieleweka (ndio)
sasa hivi yamebaki majina

mna shobo kwa presenters mnapelekwa na media
nyie wadogo kwa presenters mnavyoteswa na media
hadi huruma miaka mingi kwa game
bado mnateseka mnasaka kipimbi fame

huu ni muda wetu kimepita kipindi chenu
zitakuaje nyumba zetu tukifuata misingi yenu?

najiuliza tu, kwenu jealousy ni tatizo
hamuoni khaligraph hivyo ndio legacy ilivyo

sisemi muanzishe labels au mfanye cyphers
au mtubebe kama stoner anavyobeba lighter, nah!
(nah)

siwafundishi kuwa ma’legend
ila ukishindwa kuwa papa nakurudisha kuwa perege

bado mna usela mavi mnapiga milege
na jinsi mnasota kutoka, sasa fiva iweje?

hii sio diss ni disconnect kati ya zao na nilipo
wala sio fix, ukitaka correct nifuate nilipo

halafu sitaki co-sign, msaada, ushauri, ujiko
kitachowaepusha na hizo aibu ni kaburi na kifo

no hard feelings my people
hip-hop ni expression, leo nakiwasha zaidi ya jiko
najua, mkubwa hasemwi hata akijamba
nimeamua mkimaindi nifuateni mi nipo mwanza

navyorusha hili kombeo sio la mwisho au la kwanza
mna stress hivyo vileo kwenu suluhisho la kwanza

i got no problems to be the villain
kila zama na nabii, wa sasa sio zama zile

sasa kuna dokta mwaka tushamsahau ambikile
hivyo idea mkitaka mtanifuata niwaandikie, what’s up

mh! mh! to whom it may concern you know
to whoever fits the description

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...