letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de niachie mimi - shah bang

Loading...

[intro]
yoh yoh, r city baby, hazard, masebo
shah-beezy, shah bang, tarakimu, salmin swaggz

[verse 1: salmin swaggz]
huu ni mgodi wa madini makini kuniskiliza
huyu ni salmini huamini au unajiuliza
anaimbaga nini mi naona kama huaga anaigiza
-n-leta story na swagger za tambwe hiza
nilianza kufoka kabla hata hujaanza kukaa
hujui nlikotoka unadata na jeans niliyovaa
watu walishoboka kabla hatujatoka kitaa
siku hizi nmeacha k-moka mtaani wameshaichoka bidhaa
we “street certified” kitaa kishatupa ridhaa
kila mahala kuna ghala la kuficha silaha
mi naongoza huu msafara bila babu na slaa
imani haiko kwenye sala tunahesabu masaa
niulize mimi, ka demu wako akitaka kuaachiwa ulimi
muulize, je ni yakini anataka kuachiwa ukimwi?
dhiki baraka kw-ngu unataka uniambie nini
game ni kibaraka w-ngu ukishindwa niachie mimi…

[hook: shah bang & tarakimu]
yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi
nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi
una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja
wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi
(repeat)

[verse 2: shah bang]
bora uniachie urithi wa amani moyoni mw-ngu
sio matamanio ya kijinga yaathiri maisha yangu
usiniachie ukimwi j-po nna pesa ya kuhonga
usiniachie mademu j-po nna uwezo wa kugonga-nisha
gl-ss za wine, it’s time to shine
uzuri sio umbo ni tabia na hulka
skiza hizi tungo ujiepushe na ufuska
niachie bili ya uzima mi ndo ntailipa
utukufu wa roho mbinguni mambo yatajipa
niachie rap niachie chap i’m in top
niachie mimi niwaulize waliofeli walijiandaa
au kile walichosoma wizara ilikikataa
uchakavu wa maisha kitaa, ni mazoea
dhambi ya mlalahoi ni story ya babu seya
mbegu waliyoipanda tayari imekwisha stawi
taaluma hazifanya kazi ila kutafutana kwa uchawi..

[hook: shah bang & tarakimu]
yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi
nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi
una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja
wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi
(repeat)

[verse 3: tarakimu]
niachie mimi, bingwa wa biashara
ambaye najiamini, na naipinga hasara
mjasiria mali niliyejawa ubunifu
kila saa niko tayari kukabili kila kitu
niachie utafiti, nikupe matokeo
nna mbinu ya kudhibiti uhaba wa pembejeo
nina uthubutu, akili sio butu
natumia mawazo, mtaji na sio mtutu
najua bidhaa, bei, banda na bango
daima sikosei nimejipanga kitambo
hua naficha mia kila nikipata mia mbili
hakika nimepania mpaka waniite tajiri
nakopa kwa fursa, nalipa kwa wakati
naogopa kuvaa supra, riba itanish-taki
ukipata kidogo bwa’mdogo acha dharau
maisha yakikupa kisogo chap tutakusahau

[hook: shah bang & tarakimu]
yako tatu, yako mbili ila moja…niachie mimi
nenda mgambo, sungusungu, u-soldier…niachie mimi
una hoja ya nguvu, mi nna nguvu ya hoja
wa mbili havai moja utangoja…niachie mimi
(repeat)

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...