letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de chemsha bongo - professor jay

Loading...

mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa

chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua

kwa kifupi nimekulia kwenye maisha ya kitajiri
wazazi walinipenda walinipa lile na hili
na tangu nikiwa mdogo nilionesha kwamba na
akili
sio siri nilikimbia umande kusoma niliona sio
dili
maisha yalikuwa matamu, nilisahau ya jehanam
ilitakiwa uwe na hali flani upate yangu salamu
washikaji niliwapita maskani kama vijisanamu
wazee wenye busara walisema kijana hana
nidhamu
hawakuumiza kichwa, niliamini hawatanilisha
hawatanivisha, na hawajui utamu wa maisha
mi ndo mimi mwendo mdundo, wengine niliona
uvundo
niliamini naweza kula muwa pasipo kuvuta
fundo
walisema mafumbo, fedha kw-ngu ni kama
nyundo
na kila aliyenigasi sikusita k-mjibu utumbo
nilibadili mikoko mbali mbali ya kifahari
nilikuwa napanga kreti za bia wapambe waoshee
gari
mademu walijigonga, mashangingi walinipenda
nilikuwa na toto mbili kila kiwanja nilichoenda
niliitwa millionaire bill gates, mzee wa kuku
wapambe walipepelea we we mambo ipo huku
na kila aliyenigasi sikusita k-mpatia buku
aliyejifanya kiburi hakutafuna yangu ruzuku
tulikuwa tukihama hama leo o’bay, kesho
mikocheni
nilikuwa nabadili baa leo side boy, kesho kwa
macheni
werevu walinishauri nilisema w-nga niacheni
na ka hamna shughuli kasuk-meni mikokoteni

mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua

kila club niliyoingia, wapambe walishangilia
kwa kuwa walipata hakika ya kula kitimoto na
bia
mademu waligombania, kila mmoja
kunik-mbatia
wengine walikuja kwa nyuma, “jay
tunakuzimia”
nilikuwa na desturi kila kiwanja nafunga baa
niliposema wote kunyweni bure, hakuna
aliyeshangaa
siku moja nilikuwa beach na demu mmoja
kipenda zuwana
asikwambie mtu jibaba nilikuwa na hela!
nilikuwa nimepaki mercedes benz, convertible
eboh!
ilikuwa nyeusi, rims za gold
si ya hela kidogo
wapambe walikuwa wamepamba range rover
nne nyekundu
nilikuwa naongea kwa nyodo huku nikicheka
kizungu
nilifanya vurugu ya mwaka na ushenzi
tulivyotaka
maji tunatoa juu w-ngwana walibaki nyaka
nyaka
tulivunja sheria za barabara na trafki alichekelea
alijua akizuia msafara bosi wake atamfokea
fedha iliongea, hakuna aliyenisogelea
na kila aliyenigasi aliozea segerea
ila wazazi walinihusia kwamba urithi w-ngu ni
elimu
niliamini unasoma upate fedha hivyo sikuona
muhimu
kwa kuwa nilikuwa kiburi ndugu zangu
hawakunipenda
mtukutu jeuri familia yangu ilinitenga
nilianza kula mtaji nionekane bado natesa
niliuza gari zangu tatu na nyumba nikabaki na
chaser
maisha yalianza ku-change madeni yakawa
mengi
kuna wakati nilikimbia na kwenda kujificha
zenji
viwanja nilivyozoea hivi sasa nikawa siendi
wale mademu na wapambe wote wakaanza
kuniona mshenzi
wote walinikimbia na mbaya zaidi walinicheka
walisema “cheki jay alosto ameshazeeka”
nilianza kuweka bond mpaka vitu vyangu vya
ndani
niliishi kama digidigi sikuonekana mtaani
umaskini umepiga hodi kuishi sasa sikutamani
sijui nilie na nani jamani nipo mashakani

mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua

ilitokea ajali mbaya, wazazi w-ngu wote wakafa
nikajua wataridhi mali kutokana na hayo maafa
nikajipo moyo mi ni mzuka niliyefuf-ka
ingawa nilikuwa na macho k-mbe nilikuwa
nimepof-ka
vilianza tokea vizingiti na sielewi vilipoibuka
watoto wa nje na mama wa kambo walipandisha
hulka
wajomba na mashangazi wote wakawa
wamecharuka
akili ilianza kuruka, harufu ya damu ilianza
kunuka
waligombea mali nikaona ni heri kufa
matajiri ombeni kwa mungu kabla ya siku ya
kuanguka
binadamu ni kama maua, kwani huchanua na
kunyauka
na fedha ni kama shetani ukiwa nayo huwezi
tukuka
dunia kizingiti, yataka mkono wa mungu
kuvuka
nenda kwa mapozi, mwenzio nalia
nimeshaumbuka
hapa nilipo nanuka kikwapa, sijiwezi mchafu
kunuka
mwili w-ngu ni kama kipande cha muhogo jinsi
nilivyopauka
hutakiwi kucheka, walimwengu kweli najuta
mbele ya mungu na hii dunia naamini milango
itafunguka
chini ya miguu, mwana mpotevu naanguka
bible na quran vinasema samehe anayejuta
wananchi wenye ghadhabu bado wananipeleka
puta
walitaka kunichoma moto, walishaniloeka
kwenye mafuta
fanya hasara ya kunitafuta, kila saa na kila
nukta
usitake yakukute ndugu yangu yalionikuta
yoh.

mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua
mwokozi nitoe roho niepuke hili balaa
maisha nilichezea leo hii nalala njaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukashangaa
chemsha bongo kabla hujavagaa, ukadua

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...