letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de kikao cha dharura - prof. jay

Loading...

nashukuru sana wananchi kwa kuweza kunipa kura
nashangaa nimeitwa ghafla kwenye kikao cha dharura
kikao kinaashiria kina maswali juu yangu
hii inatokana na ndio mzee na ahadi zangu
naona watu ni wengi wananchi walio na maana
najaribu kutafakari ni nini kinawachanganya
nipo tayari kujibu maswali yeni zamu kwa zamu
watako uliza maswali ningependa kuwafahamu
“naitwa sajenti bihonerwa kwa niaba ya jeshi la polisi, nilikuwa nnauliza zile helkopta zetu vipi?”
nafikiria kuanzisha kwanza chuo cha marubani
vinginevyo mtapata ajali nyingi sana angani
baskeli hujui kuendesha helkopta utaendeshaje
kila mtu aendeshe yake huko angani itakuwaje
“mweshimiwa na sisi wakulima ulituahidi matrekta, na siku zinayoyoma tu mbona hujayaleta?”
wakulima mngeendelea tu kutumia jembe la mkono
serikari haina hela bajeti imefika kikomo
naona kilimo cha mkono kinaendelea vizuri
jamani kazeni mikono еndeleeni kukaza msuli
wananchi tupo pamoja hapo (sio mzee)
watanzania tumeelewana kule (sio mzee)
washika dau na wapiga kula palе (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)
wakulima tupo pamoja pale (sio mzee)
wanafunzi tumeelewana kule (sio mzee)
mabamedi na mapolisi pale (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)
mabamedi ondoeni hofu kilio chenu nimekisikia
mabenz yenu yapo bandarini tayari yameshawadia
nimemchagua kiranja ili anipe idadi yenu
niwape funguo zenu muondoke na magari yenu
“ulituhadi utajenga barabara tano juu na chini
hizo zote hatutaki tunataka moja tu ardhini
kila siku tunapita barabara zinakuwa mbaya
umeyafumbia macho mheshimiwa uoni haya”
barabara ya makwekwe nimeshaimwaga kifusi
baada ya wiki mbili itakuwa safi kama urusi
wakandarasi wanafanya kazi kutoka china na madagascar
kuhusi vibarabara nawaomba muondoe shaka
“eh, vipi mzee mabomba ya kutoa maziwa nchi nzima?”
jamani naomba muulize maswali ya kiutu-uzima
mabomba ya kutoa maji na maziwa haiwezekani
mlininukuu vibaya nasisistiza haiwezekani
“mzee hali ni mbaya basi tungegawana vyakwako, kwenye kampeni zako si ilikuwa ni moja ya ahadi zako?”
eh, kugawana vyakw-ngu ilo swala litakuwa gumu
familia inantazama ebo nnamajuk-mu
imeandikwa kila mtu atabeba msalaba wake
kila mbuzi ale kwenye urefu wa kamba yake
mbona mnaniluliza maswali mengi ya ku nikunikomoa
jamani watanzania tunajenga tunabomoa!
wananchi tupo pamoja hapo (sio mzee)
watanzania tumeelewana kule (sio mzee)
washika dau na wapiga kula pale (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)
wakulima tupo pamoja pale (sio mzee)
wanafunzi tumeelewana kule (sio mzee)
mabamedi na mapolisi pale (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)
wafanyakazi wa serikarini sasa nyi magari yanini?
daladala chungu nzima mnaweza mkawahi kazini
nasema mnapenda sana starehe kuliko kazi
na hiyo ndio sababu mnaharibu hiki kizazi
wanafunzi niliwahaidi mtafanya practical mwezini
kabla ya kuwapeleka mi nilifanya tasmini
nimegundua huko mwezini kweli kuna baridi sana
na pia kunavitisho kuwepo kambi za osama
mkinichagua tena mta kwenda huko mapema
na nnatatekeleza kila neno nnalosema
kimsingi nimezongwa sana na haka kamuda
mkiniongeza muda kila kitu ni baab kubwa
wengi ni kimya na mswali yamepungua!
yoyote mwenye swali ningependa k-mtambua
naona mnanong’ona tu na wengi mmekunja sura
hii inaonyesha mmeridhika kunipa kura
nadhani ndugu zangu tupo pamoja (ah wapi!)
jamani punguzeni jazba basi kidogo (atutaki!)
sasa watanzania mbona mnaanzisha vurugu
nadhani mmesahau watanzania wote ni ndugu
ye-ye – ye jamani nasema hivi kikao kimehairisha
jamani maafande, afande miraji, afande mzafaru, afande nani? gondwe, njooni mtusaidie huku
wananchi tupo pamoja hapo (sio mzee)
watanzania tumeelewana kule (sio mzee)
washika dau na wapiga kula pale (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)
wakulima tupo pamoja pale (sio mzee)
wanafunzi tumeelewana kule (sio mzee)
mabamedi na mapolisi pale (sio mzee)
ehh (sio mzee), eti (sio mzee)

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...