letra de natoka tanzania - nikki mbishi
intro:
ngwessa
natoka tanzania
(yea,yea natoka tanzania) yea, tamaduni muzik baby
(wakilisha) unju bin unuki (nchi yetu tz bongo) naipenda tanzania
(jamani karibuni tufanye utalii wa ndani au sio…)
yea 1,2 1,2 we don’t stop til’ the music…
(..wanyama wapo mtaani siku hizi hawakai mbugani tena)
verse i:
(yea) nchi ambayo haithamini mchango wa sanaa
wanaoitwa wasanii, mitaani wanakufa njaa
bongo fleva ni utumwa
ndiyo maana machizi wanajituma kusuk-ma madawa ya kulevya (wanyama)
tony montana, noriega
pesa motivator, nicheki kwa sony wega
nchi ambayo, stori ndogo ni gumzo kwa taifa
nguza, papii kocha jela kifungo cha maisha (aiyaa)
nasema ukweli, tindikali si hofii
wezi wa rasilimali za serikali wako free
wako hai kimwili, kiakili wameshakufa
hata hoja fupi wataijadili hadi kesho kutwa
nchi ambayo, mpaka mortuary wanaomba rushwa
traffic na dereva, polisi yuko kwa pusha
wako ghetto wana moka cha dom na cha arusha
na ukiongea umbea tu, umesutwa!
hook:
ayo, natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
verse ii:
nchi ambayo, raisi ni mzito kwenye maamuzi
anafumbia macho vigogo na walanguzi
vya msingi nyuma, vya mbele ni vya kipuuzi
na juzi, alikuwa kwenye msiba wa bongo movie
nchi ambayo, falsafa hazina tafsiri
kwenye shule za kata hakuna mtoto wa waziri
tunasoma sisi tu
tun-z-di ku-potezwa mithili fisi ndani ya misitu
mashabiki wanapenda flow za nikki
wanahoji vipi? mbona si sikiki, tuzo hamnipi
nikidiss wanasema natafuta kick
nchi ambayo 50 cent -n-lipwa mimi silipwi
kama unapeta, peta ila jichunge
ukitaka kuwa shetta nenda kwa chief kiumbe
nchi ambayo ma-meneja ni ma-damager
eti, trap beats ndiyo kipenzi cha ma-teenager
hook:
ayo, natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
verse iii:
tanzania, wala si msanii jamani
kama ni uzalendo tuanze na utalii wa ndani
nchi ambayo sista du hajui emcee ni nani
field marshall nawachora ma-mp vitani
nijenge nikujenge, tujenge na tupendane
siyo una-like fan page yangu ili unitukane
au nifanye kama dimpoz nadai
nikate mauno, rich mavoko, bolingo nangai
nchi ambayo wawekezaji imewabidi kusanda
mashoga kibao, bongo umagharibi umetanda
sababu ya joto, hasira in-z-di kupanda
“stay positive” aliniambia fareed kubanda
karibuni tanzania, wazungu, walatino
wa-dutch, wazulu, waarabu, wafilipino
toka ukonga ya ilala, temeke wapi kino
na ukitaka ganja kali ni sinza kwa cappacino
hook:
ayo, natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
natoka tanzania, tz bongo
nchi ambayo viongozi wana-cv za uongo
asilimia 70, wananchi ni maskini
kaa chini fanya tathmini, niambie unacho ona nini
outro:
yea, niambie unacho ona nini
nikki mbishi baba malcom
unju bin unuki, zohan, ??
baba bomba, utingo tishio jogoo
majina kibao, nipo na ngwessa au sio
hii ndio ile nchi bwana
shabiki ana-like fan page yako facebook
anaku-follow twitter, instagram ili akutukane sio
badala ya kukushauri akujenge
sikilizeni nyie, ukitoa maisha ya kwenye media
tuna maisha binafsi pia
kwa hiyo tusifwatiliane kupita kiasi ,au sio
ehh, hii dunia tu, dunia njia
na dunia ni gunia, na gunia halibebi maji
au sio, ahsantee
letras aleatórias
- letra de мы в деле - band lb
- letra de noms [n*ggas on my side] (ft. rae carti) - thomson nasser
- letra de memories of you - murder at the dance club
- letra de putting up - christian rowell
- letra de keeper of the vision - pam mark hall
- letra de paradigm ritual - first signs of frost
- letra de karma - kjento
- letra de california poppy - theo lawrence
- letra de faded star - beccy cole
- letra de renew me - emma bradley