letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de nalivua pendo - mwasiti

Loading...

[verse 1]
leo nalivua pendo nililopenda zamani
nabadilli w-ngu mwendo nami niwe furahani
nimechoshwa na skendo, vita na purukushani
kweli asiyejua pendo apendwapo hapaoni
nilimpa kwa kishindo penzi lote la moyoni
raha na wingi uhondo sik-mnyima mwandani
ameyavunja kwa nyundo mwenzenu sikuamini
leo nalivua pendo nirudi yangu thamani

[chorus]
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo

[verse 2]
niliyajenga kwa nondo mapenzi yangu ya ndani
kwa ufundi na miundo na mambo yote ya pwani
k-mbe nalea uvundo aibu tupu nyumbani
kweli asiyejua pendo hapendeki ni shetani
pendo gani la magendo apendwae hafanani
leo naliweka kando pendo hili la kihuni
najiepusha na lindo k-mlinda hayawani
kwani mapenzi mkondo hayataki ushindani yeah
[chorus]
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo

[verse 3]
nimehitimu msondo, msondo wa kizamani
nikahusiwa upendo, upendo siri yake nini
nimefundwa kimitindo, na starehe za chumbani
kupendana ni matendo, mtendeane hisiani
kweli mchezea jando, mapenzi kwake ni nini?
bora niyapige tindo, mimi nawe buriani

[chorus]
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo
ada ya mja hunena, ungwana ni kitendo uuh
hadhi yangu kubwa sana si mimi kuwa mdondoo
hatuwezi kulingana kauli hata matendo
kwaheri ya kuonana leo nalivua pendo

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...