letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de tulizana - mbosso

Loading...

eeeh, mmmh, eeh
ana vidimple dimple
vishimo shimo mashavuni
mikononi vipiko piko
eti kipini kipo kitovuni

ya nini nibaki kiwiliwili
na kichwa changu ni wewe
iweje pendo kwao liwe pilipili
na twakula wenyewe

mungu kakuumba
mithili ya malaika yayaya
samaki wa kukunja
chumbani unanyumbulika yaya

kwa penzi usitie kibanzi
kitaniumiza ah
upendo ukawa kitanzi
nikajining’iniza

ikienda mrama irudishie
(popoa popoa dodo)
ikikwama kwama isuk-mie
(popoa popoa dodo)
tulizana
tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane

kama nyota na mwezi
vilo mwana na angani
tung’arishe penzi letu sote
tupeane penzi bila choyo chochote
na bila hiana kwetu sote

elewa mapenzi ni chombo
kinachotuunganisha
ni chombo kinachosafiri
kati ya mioyo yetu miwili ilofaidi

tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane
tulizana mpenzi tupendane

ikienda mrama irudishie
(popoa popoa dodo)
ikikwama kwama isuk-mie
(popoa popoa dodo)

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...