letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de ndoto ya mchana - ksonrap

Loading...

[intro]
this one right here is for the people
nimelala mchana nikaota
yeah, let’s go

[verse1: ksonrap]
ajira hakuna tunasuk-ma mikokoteni;
wanasiasa baada ya kampeni wameingia tu mitini;
bila hata kandili wametuacha tu gizani;
hakuna kufanya mikutano chama cha upinzani;
kila kitu wametupiga pini wanasingizia vita vya ukraine;
vitu vinapanda bei madukani nachokisema nikweli wala sio utani;
hali mbaya wafanya biashara wan-z-funga tu mizani;
shekhe msikitini anakosa hela yakununua hata ubani;
hakuna anaetoa sadaka kanisani hatuna hata mbuni;
hakuna madawati watoto wanakaa chini mashuleni;
sare zao zimetoboka matakoni;
wabunge wao wanasinzia tu bungeni..
new model land cruiser wan-z-paki tu uwani;
sisi wametuacha kwenye mataa haliduni;
wanaishi zao tu mijini tuvyoishi ni kama mateka tu vitani;
hakuna madawa hospitalini bima ya afya akupe nani?;
majisafi hayatoki mabombani;
hawachimbi visima eti umekauka mto wami;
siku hizi hakuna bunge live kideoni;
huu mwaka wa ishirini bado mnatuahidi mtaweka lami;
lawama tumpe nani?
wanapitisha tu kokeni mateja wan-z-di tu kujaa mitaani;
magendo yanapita tu bandarini hatupo hata makini;
wanasafirisha makinikia watuambia sio madini;
ndege zinatua wanyama wanaibiwa tu porini;
nyie kopeni cag anatuambia yanaongezeka tu madeni;
nduguzao wanawateuwa wapo wilayani madaraka yashawalevya kwani mtawafanya kitu gani;
wanaharakati na watetezi wote wapojela wanakesi za uhaini;
waliponea chupuchupu walikimbilia uhamishoni;
ukizungumzia katiba mpya wanakutia tu mbaroni;
hii ni ndoto nimeiota mchana kweupe wala sio jioni;

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...