letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de barua - j 93

Loading...

verse(j93)
barua naandika kwako mama
napenda nikwambie nimekuk-mbuka sana
ni miaka mingi ila naona kama jana
pasipo uwepo wako maisha hajawahi fana
machozi yananitoka kila nikik-mbuka
mambo yalichange mama tu ulivyondoka
familia yetu ikaanza gawanyika
kwasababu kwenye nyumba yetu tulitoka
mjomba na shangazi walitutimua
siku hiyo dada t sana alilia
njia panda hatukujua pa kuelekea
kwa sauti nikalia uweze kurejea
siku hiyo tukalala nje ya nyumba
hakuna usingizi hata macho sikufumba
balaa la baridi mpaka mbu wakatuk-mbuka
asubuhi tukafika kwa uwezo wa muumba….

chorus (shine nuny)
nikweli umekwenda na j-po hatukupenda
ila mungu kakupenda najua…
masiku yamekwenda na muda umepita leo kwako naandika barua…
barua kwako mama, najua upo salama…

verse 2
walisema yanafurahisha yajayo
ni usiku wagiza usilijualo
ni mabaya mengi mama yapatayo
ila leo naomba nikueleze yafuatayo
gari yako mama pia waliuza
mjomba wa kawe na shangazi wa buza
nilipigwa kofi nlivyotaka kuuliza
hata senti tano tupatia hawakuweza
naomba nikuambie ndoto yangu haikutimia
mimi kuwa daktari ulivyopendelea
nilikwama ada sina wa kunilipia
shule nikashindwa fasta wakanitimua
mama nimemis msosi wako
chakula ni mabaki ndio nakula tu mwenzako
rudi hata kidogoi nikuone mtoto wako
ninakuombea huko mama uliko

chorus (shine nuny)
nikweli umekwenda na j-po hatukupenda
ila mungu kakupenda najua…
masiku yamekwenda na muda umepita leo kwako naandika barua…
aah aaah ukiapata muda uisome
aah aaah ukipata muda uisome
barua yanguu uuuh uuh
barua yangu …..
barua kwako mama
najua upo salama….

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...