letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de bwana - gelax wakristo

Loading...

intro
wakristo……
wakristo……..

chorus
halleleluyah hakuna kama wewe x2
mbingu na nchi zimejaa ukuuu wako
hakuna kama wewe eeh

verse 1
wewe ni bwana pekee
umenifanya ibada hakuna kama we
unayaweza yote duniani na mbinguni
unatawala kote
umeonyesha pendo kwa vitendo
neno la msalaba tuna amini unatupenda
nakuita baba bila siwezi kwenda
tujaze nguvu hatuijui kesho
leo tu udumishe wokovu wa siku ya mwisho
ni haja ya moyo uwe na sisi
tuko hapa ufalme wa mbingu kuuakisi
tukikupendeza tukienenda kwa imani
mapenzi yako kutimia furaha toka ndani
roho yangu hii hai sababu yako
adhama sifa muweza vyote ni vyako
nakuhitaji,muumbaji
nakutii mwisho univike taji

chorus
ni wewe tu bwana, hakuna kama wewe x2
mbingu na nchi zimejaa ukuuu wako
hakuna kama wewe eeh

verse 2
mungu wa ajabu haufananishwi
akili zako ni kuu hazichunguziki
yehova rafah ndiye mponyaji,wewe ni alpha
(umeketi juu ya kiti cha enzi
mamlaka ni yako hakuna ambacho haukiwezi,) x2
bwana wa majeshi katikati ya wenye heri
asante kwa roho atupaye uzima na kweli
kwa agano la roho ametufanyia wepesi
naenenda kwa roho sheria ya mwili haina nafasi
bwana yesu ndiye mwamba wenye kinara
niko naye sintoogopa n-z-fuata ishara
utakatifu ni hekima iliyoshuka
ukombozi ni haki nilioipata
leo ni mwana wa mungu aliye juu
napata mema tangu nilivyo wekwa huru
mpaka kuingia mji ule wenye nuru
usinipite , uniguse bwana unapokuja zuru

chorus
ni wewe tu bwana, hakuna kama wewe x2
mbingu na nchi zimejaa ukuuu wako, x2
hakuna kama wewe eeh

verse 01
kwangu yesu wewe ni mwamba imara
wokovu wangu kwako mimi nitazama
ufunuo wa neno jaribuni siwezi kwama
ndio nguvu yakushinda uovu katika ujana
usaidizi madhubuti kutoka kwa roho
umenitendea miujiza ushuhuda huo ninao
mwili wangu ni hekalu kwako liwe kao
imani niliyoisikia kwangu ndio ngao
tu nikae na wewe milele yote
furaha na amani niliyoipata nisiikose
wenye mizigo waje kwako uwatue
bwana wa mabwana kila mtu akujue

chorus
halleleluyah hakuna kama wewe x2
mbingu na nchi zimejaa ukuuu wako
hakuna kama wewe eeh
wakristo…
wakristo……

kessy harmonizing…………

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...