letras.top
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

letra de starehe - ferooz

Loading...

[chorus: ferooz]
hapa nilipo mimi nipo kitandani
starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
masela w-ngu, ndugu zangu buriani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
sewa side, scout jentaz ‘kwaherini
bongo records na majani ‘kwaherini
hamtoniona tena duniani
sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
ibilisi amefanikiwa kunivuta
sasa sijui wak-mlaumu nani ‘kati ya nafsi yangu ama shetani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
makongo na jite ute, kwaherini
(?) na azania, kwaherini
ah aah aaah…

[verse 1: ferooz]
ni saa saba juu ya alama saa nikiitazama
nimesha achana na jackie sasa namfuata salama
saa k-mi na mbili na appointment na mademu wawili ‘achana na lily ambaye tutakutana saa mbili
jane wa mikocheni ambaye sasa hayupo duniani aliye kuwa akinisubiri pale vaticani kijiweni
minah na s-m-ni tunakutana kwa macheni
na kila siku niliwabadilisha tena kwa foleni
huo ndio ulikuwa mwenendo wa maisha yangu, mimi viwanja kujivinjari na machangu…
oooh, niliona fahari… yeah
starehe mi nilizifanyia papara, nilibadili mademu kama vidaladala
nikienda nimepanda hili, nikirudi lile ‘nilitamani starehe zote nizitawale
hata k-mk-mbuka mola w-ngu ilikuwa ndoto
nilitekwa na ulimwengu k-mbe na ukimbilia moto
tabia za kubadili wasichana nilikubuhu
nilitembea na watoto wa geti, machangu na ma-sista doo
ubaya kwamba condom sikuitambua
kwa kujua kwamba ladha ya mapenzi itapungua
k-mbe nilikuwa ninapotea njia ‘nlioshauriwa mimi nikapuuzia
idadi ya wanawake ikawa lukuki, ikapita kipindi wengine nikawa siwak-mbuki
ona, ona…
ona sasa yaliyo nisibu kwa dada yake bashiri
nilishamsahau kama tulishakutana kimwili nilivyo muona nikamtongoza tena, tena kwa mara ya pili
ona sasa, ah aah aaah
[chorus: ferooz]
hapa nilipo mimi nipo kitandani
starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
masela zangu, ndugu zangu buriani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
afande sele ‘morogoro, kwaherini
arusha, wanapolo, kwaherini
hamtoniona tena duniani
sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
ibilisi amefanikiwa kunivuta
sasa sijui wak-mlaumu nani ‘kati ya nafsi yangu ama shetani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
discipline camp na wa kush, kwaherini
sinza star na choka mbaya, kwaherini
ah aah aaah

[verse 2: prof. jay & ferooz]
kijana vipi?
mbona hujagonga mlango?
jipange kwenye foleni, mmoja mmoja ndio mpango
ondoa mashaka tiba bora haitaji haraka
subiri watibiwe wenzako nawe utafata
dokta, mimi nimekuja kufanya hitimisho, naamini hii ndio itakuwa ungwe yangubya mwisho
dalili zinaonesha nimeathirika na nimekuja pima tu nipate uhakika
ebu cheki dokta nilivyo konda, nimebakia mifupa, mwili umetapakaa vidonda
vipele usiseme hii yote dalili ya umeme, dalili ya umeme…
no! acha uoga hata malaria iko namna hii
unaweza ukakonda kwa typhoid au t.b
ukinificha una hatarisha maisha, ni bora kubainisha kipi kinakutisha, eh?
homa za mara kwa mara kw-ngu hazikatiki, kuharisha mara sitini na mbili kwa wiki
eenh angalia hata nywele zilivyo nyonyoka, mabega yamepanda juu utasema yanach0m-ka
ninao, ninao
supiri vipimo!
ninao, ninao
usikate tamaa!
ninao, ninao
dokta usinipe moyo, ni sawa unampa mfupa autafune kibogoyo
duniani mimi sina umuhimu, kuiaga dunia inapaswa, ina nilazimu
ni bora nijue tu, nielekee kuzimu
no!, no!, hayo ni maamuzi ya ajabu, na ni ulimbukeni kujiua pasipo sababu
maradhi ni kawaida kwa binadamu hilo fahamu
ni vyema ungetulia upate majibu ya damu
sasa k-mbe wewe unaona mimi nasubiri nini, ni bora tu niwahi kupumzika kaburini
starehe mn-z-penda ila mwisho wake mbaya, wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya
vipimo vinaonesha ni kweli umeathirika, i’m very sorry, kupoteza nguvu ya taifa
ni vyema kufanya ibada na k-mrudia muumba wako, kula vizuri, fanya mazoezi, pumzisha mwili wako
ukizingatia hayo utaishi kwa matumaini
by the way, unayo nafasi hebu jiamini
mola aliye niumba sasa nishamkosea, ( pole kijana )
hata ardhi na mbingu zote zinanizomea, malaika wa zamu kwa hamu wananingojea
nikifika huko nani atanipokea…?
ah aah aaah
[chorus: ferooz]
hapa nilipo mimi nipo kitandani
starehe zimeniweka matatani, kupona tena haiwezekani
masela w-ngu, ndugu zangu buriani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
wa bara na visiwani, kwaherini
t.m.k., kino plane, kwaherini
hamtoniona tena duniani
sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
ibilisi amefanikiwa kunivuta
sasa sijui wak-mlaumu nani ‘kati ya nafsi yangu ama shetani
kwaherini
kwaherini
kwaherini
kikosi cha mizinga, kwaherini
migo migo sinza, kwaherini
ah aah aah
ah, ah

( instrumentals )

letras aleatórias

MAIS ACESSADOS

Loading...