letra de hatia vi - dizasta vina
salamu baba mi mwanao
naandika waraka kwa maana hutaki vikao
nahitaji majibu nikihisi ni haki yangu
najisikia vibaya kusikia unaishi na sina ngao
nimeshika kalamu haya maandiko
yametoka mahala timamu palipo wito
sijatumwa na wenzangu hii ni akili yangu mwenyewe
waraka huu ni salamu zangu za mwisho
nina akili najua mambo yanapokuwa mrama
natambua uhalisia n-z-tambua njama
pengine nitachokisema kitazua laana
nitaibeba lawama kwa kujifanya najua sana
ndugu zangu wanachosema sisawiri
mpaka wanahisi nimeanza kuchezwa na akili
hata wakitaka kunitenga sibadili
ulinitenga jana siogopi kutengwa mara mbili baba
majirani wanatamba kukuongelea
wakisema sina baba na kazi ya kukusemea
na ukweli ni kwamba ni utata sana kukutetea
maana shida ilinibana na baba haukutokea je
utachukia nikiegemea penye power
au utanipa hatia mikono michafu niende nawa
nipo mbele yako kamwe siigizi uwepo kama wewe
basi jibu kero zangu twendе sawa
juzi nilikuhonga maua, jana nikakuhonga na tena
subira gani isiyo na heri shaabash
nimechoka kuchomwa na jua
jionyеshe leo nimechoka barua
nimechoka barua
barua zako zinahubiri ushindi
kutangaza vita wakati mtutu tu haushiki
na cha ajabu maadui ni wa kurithi
chanzo ni kitendawili nilichokisoma kwenye hadithi
njoo ulee wagonjwa ndo’ uongee kuhusu upendo
tuvae bendera moja ndio uongee kuhusu uzalendo
msamehe aliyekufanya uondoke ndo’ uendeelee
kuhubiri kutubu kuhifadhi na kusamehe
jenga daraja baba mahusiano yanavunjika
hamna faraja huoni wanao wamekaza ndita
jenga imani tena kwa wote waliogadhibika
jenga kama ambavyo uliijenga hii nyumba kwa siku sita
haukuja tulipopita kwenye
miaka 400 ya utumwa njaa maradhi vita giza nene
nipe sababu moja vipi nikujali vipi nikupende
sababu moja tu kukusikiliza wewe
nyumba uliyotupa ina twiga ina ndovu
majirani warembo wenye figa na vitovu
vinavutia, kuna dhahabu kadhalika
zinatutajirisha ila zinafanya tuwe waovu
huu uchafu atatetea wakili gani
siri ipi na asili zetu hazilingani
j-po akili mali sio siri asili ghali
tunamwagana damu kugombea rasilimali
tunaisha kwa wivu wetu
tunasita kwa uvivu wetu
tun-z-kwa na mbinu zetu
tunapikwa na kinu chetu
tunasita kushika insha
tunapitwa na wapita njia
umoja unavunjika huku
tumeshikwa na simu zetu
sina tofauti nna watoto kama wewe
napata changamoto kama wewe
kama soja kwa ajili yao napambana naposhindwa
tunateseka pamoja kwani sina roho ndogo kama wewe
asante kwa ulezi dhanifu
asante kwa kuniandikia sheria za kishenzi
kwenye pegi nadhifu asante kwa kuniacha stendi
nikisubiri mapenzi ya ahadi nakesha nikienzi wasifu
asante kwakuwa mbali nami
kiasi nina shaka kuwa haujui nina hali gani
umeacha barua ndefu ambayo sijui kama yako
au ya kufoji na bado inahitaji mkalimani
ona napanga mipango ya kijinga
ona naghafirika nafanya uliyopinga
ona napinda napika chuki wenzangu
wenye nyumba ndinga maana mimi ngano tu inanishinda
huko mbali umejitenga nashanga
haujui kinachosemwa na jamaa
haujui usafi ni ndoto, ndoto iliyotengwa na ridhaa
haujui ni ngumu sana kuwa mwema ukiwa na njaa
haujui kuhusu adha za dunia
haujui kero maana maudhi yalipokupata ukakimbia
haujui kuhusu kifo na magonjwa haujui kuhusu
insha na maandiko haziwezi tibu hivi vidonda
ndugu zangu umewajenga kwa vpaji
wapo kadhaa umewapa pesa za mitaji
wengine warembo wenye vyeo wenye hadhi
sisi tusio na hali tulalamike kunyimwa haki
imechaf-ka taswira inaenda slow focus
pengine its all bogus
pengine i’m mad
and i’m talking to my own conscious
labda haupo ni hadithi tu
na kama ulifikia kifo ufalme umefika mwisho
haurudi tena so nawaza
lini utakuwa mwisho wa uhanithi huu
uzazi sio simple but i still care
nina watoto shida zipo and i’m still here
matatizo yanapokaba kwenye shingo sikimbii
napambana mpaka mwisho like a real man
sio kosa langu kutokuwa na uhakika upo
sikujui sura maana hauna picha google
nipe ishara kuwa unaishi hata nikituma
bakshishi niwe ninajua kuwa zinafika huko
wenye majoho rangi nyeupe na dhahabu
wana barua zako za tafsiri za kiarabu
wanasema wanakujua kuliko ninavyokujua
nikiwatilia shaka wananiita mwanaharamu
je ni kweli uliwapa uwakilishi
ni ngumu kuwasadiki hasa ukiwadadisi
kama wanaongea uhalisi au wanachonga sera
sometimes hawafundishi wananiomba hela
thibitisha hizi hifadhi si uwongo
uliowaacha wana nishani za uozo
wakificha sura kama ulivyoficha wewe
utawaadhibu kwa maji na moto
wakati unahubiri msamaha
nina maswali bado
halahala sikukemei
nashangaa wenzangu wanakesha
wakiimba utukufu wa dhambi zako
au ndo’ mkubwa hakosei
nimeelemewa na dhambi
baba mzazi unasema sina hadhi
unajua wasifu unajua majibu
umenizaa dhaifu unategemeaje niwe msafi
kwanini usije ili tujue moja
uuonyeshe uso wako ili tufunge hoja
kwanini usijionyeshe tufurahi nafsini
tujue kipi halisi kipi soga
wanao wanaweka mipaka wakivutana
wanabishana kila kikao wakikutana
wameishi bila uwepo wako juzi na jana
swali ni kwamba utaonyesha hasira wakikukana
ulinizaa kwa matakwa yako
nilisimama kwa ajili yako ni zamu yako leo usimame kw-ngu
sina usafi kama wako hautaki nilitaje jina lako
kwanzia sasa usilitaje langu
nilihitaji jibu moja tu sio picha mia
umeamua kujificha so najificha pia
nimekutafuta vya kutosha nimechoka
nipo hapa ukinihitaji unajua pa kunipata dear..father
letras aleatórias
- letra de bien visual - dogos
- letra de larry flynt - cee
- letra de hurt again - beren olivia
- letra de prove - hill view #73
- letra de memories... - cairo!
- letra de done - mista max
- letra de words - carvakas
- letra de fuxmas - twominuteshate
- letra de my bubblegum - gregory mann
- letra de skit 6 (blady król) - bisz